Walter Chilambo aitaja hofu aliyonao kuachia wimbo mpya

Walter Chilambo ana ngoma kibao alizorekodi lakini anahofia kuziachia kwasababu hana management.
Mshindi huyo wa BSS amesema kuwa hiyo ni hofu yake kubwa na ndio maana amekuwa akiachia tu cover kwa sasa kwasababu hana cha kupoteza. “Sasa hivi sitaki kabisa kuwaambia watu nitatoa lini sababu nimeshaongea sana nitaonekana muongo ndio maana nimetoa cover hiyo watu wajue nipo naweza kufanya kitu lakini soon naweza kufanya chochote muda wowote.” Wiki hii Chilambo ameachia cover ya wimbo wa Ben Pol, Moyo Mashine.

0 maoni:

Chapisha Maoni