M-Rap adai ameshindwa kuwa uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzie
Rapper M-Rap amedai kuwa ameshindwa kuwa na uhusiano na msanii mwenzakeRapper huyo alikuwa na uhusiano na muimbaji, Miss Rizy lakini tayari wameachana. Ameimbia Bongo5 kuwa sababu ya kuachana ni kushindwa kwenda sawa kwenye mstari mmoja.
“Nimeona bora niepuke hilo kabla haijawa kuwa hatari kubwa baadaye watu wakaja kusikia tunagombana kabisa ile, nimeona bora kila mtu sasa hivi afanye mambo yake,” amesema.
Hata hivyo kuhusu kazi amedai kuwa haijaathiri chochote kwakuwa wote wapo kwenye management moja, Mukii International. M-Rap na Miss Rizy waliwahi kufanya wimbo uitwao Hawajui.
0 maoni:
Chapisha Maoni