Rapper Kid Cudi kuonekana katika msimu mpya wa ‘Empire’

Rapper Kid Cudi amepata shavu la kuonekana kwenye show kubwa ya muziki na maisha ya “Empire.” Staa huyu ataigiza kama Gram, rapper ambaye hana lebo na atakuwa mpinzani mkubwa wa Hakeem (Bryshere “Yazz” Gray) kwenye studio na kwenye maisha.
Gram pia atakuwa ana mahusiano na Ex wa Hakeem, Tiana (Serayah McNeill) katika Empire. Kipindi cha nyuma Kid Cudi aliwahi kuigiza kwenye filamu kama Entourage na James White. Msimu huu tatu wa Empire utaanza kuonekana kuanzia Sept. 21, huku pia wakiwemo French Montana na Birdman.

0 maoni:

Chapisha Maoni