Kocha wa Chelsea Antonio Conte, amesema kiungo Cesc Fabregas bado ana mipango naye licha ya kutompanga kwenye mchezo wa jana wa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham, katika uwanja wa Stamford Bridge.
Cesc Fabregas
Bao la Costa, kunako dakika ya 89, liliihakikishia Chelsea pointi 3 muhimu, baada ya James Collins, kusawazishia West Ham, wakati Eden Hazard alikuwa ameshaandika bao la kwanza kwa The Blues kwa njia ya peanati.
"Inaweza kutokea kwa mchezaji yoyote kumwacha kwenye kikosi cha kwanza, kama nilivyomwacha Fabregas, muhimu kuona hilo ni jambo jema, kwa sababu ni lazima tupigane kwenye msimu huu, na muhimu kukaa pamoja kwa kila hali".Alisema Conte.
Fabregas aliyeachwa kwenye benchi, amekuwa akihusishwa na kutaka kutimka kwenye klabu hiyo ya darajani ambapo inasemakana huenda akakimbilia vilabu vya Real Madrid, Juventus au klabu yake ya zamani, Barcelona
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Sala sala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia hali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli kushoto akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam walipokwenda kumjulia hali. Kulia ni mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Spika Sala sala jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Sala ya kumuombea Waziri Mkuu mstaafu John Samwel Malecela pamoja na mkewe Anne Kilango Malecela.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai wakati alipokwenda na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU







Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza  tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi.


Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na  marejeo yake ya mwaka 2002,  kifungu cha 178 (1) na  (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama,  kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo  bila kibali kutoka kwa  Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kufuatia  kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua  hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.
Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia  mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na  majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama  kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.
 Imetolewa na:
Advera John  Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
                                                        Makao Makuu ya Polisi.     
Kampuni ya Google imezindua programu yake mpya kwa jina DUO. Programu hiyo ni jibu la Google kwa programu nyengine kama ile ya Apple ya Face Time,Skype ya Microsoft na Facebook messanger.


Programu hii haina tofauti kubwa na programu nyingine zinazotoa huduma za video, isipokuwa inakupatia uwezo wa ni nani anayepiga simu hivyo basi kumpatia mtumiaji fursa ya kuamua iwapo ataipokea simu hiyo au la. Programu hiyo mpya iliotangazwa mwezi May imezinduliwa kama huduma ya bure kwa simu zinazotumia Android pamoja na simu za Apple za iPhone.
Simu zinalindwa na haziwezi kudukuliwa na video hubadilika kulingana na kasi ya kushika simu inayopigwa. Kama programu ya FaceTime, duo inahitaji nambari ya mtu ya simu kuunganishwa. Huduma nyingine zinahitaji mtumiaji kuingia katika akaunti zao ili kupata fursa ya kupata huduma hiyo.
Klabu ya Everton imetangaza kumsajili kiungo Yannick Bolasie kutokea Crystal Palace kwa ada ya pauni milioni 25.
Mchezaji huyo kwa kimataifa wa DR Congo,27, amesaini mkataba wa miaka mitano kunako klabu hiyo.
Marekani imetangaza kuwahamisha wafungwa 15 waliokuwa kwenye gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba na kupelekwa Emirates.
Taarifa ya kuhamishwa kwa wafungwa hao imetolewa kutoka makao makuu ya jeshi la nchi hiyo lililopo Pentagon na kati ya wafungwa hao 12 wanatoka Yemen na watatu Afghanistan.
Kundi la watu hao ni moja kati ya kundi kubwa la wafungwa kuwahi kuhamishwa kutoka kwenye gereza hilo chini ya utawala wa Rais Barack Obama tangu mwaka 2008. Mpaka sasa idadi ya wafungwa waliobakia kwenye gereza hilo imefikia 61 hatua ambayo imeonekana kupingwa vikali na Chama cha Republican chini ya mgombea wake Donald Trump.
Hata hivyo mara kadhaa Rais Obama ameeleza masikitiko yake juu ya msimamo wa chama hicho wa kupinga mpango wake wa kutaka kufunga gereza hilo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyowahi kuitoa wakati wa kampeni za Urais.