‘Sawa Na Wao’ ya Lady Jaydee imetayarishwa na member wa kundi la Sauti Sol
Kundi la Sauti Sol la nchini Kenya linaundwa na vijana wanne ambao uwezo wao hauishii tu kuwa waimbaji. Savara na Fancy Fingers (muimbaji na mpiga gitaa wao), ni watayarishaji wakubwa. Na Lady Jaydee amedai kuwa wimbo wake mpya ‘Sawa Na Wao’ umetayarishwa na Fancy Fingers.
Kabla ya kuachia wimbo wake mpya Ndindindi, Jaydee alizunguka katika nchi mbalimbali zikiwemo Kenya na Uganda kutayarisha nyimbo za album mpya Woman.
Ni katika kipindi hicho pia ndipo alipoingia kwenye studio za Sauti Sol kutengeneza wimbo huo wa pili kutoka kwenye album hiyo.
Album ya Woman inatarajia kutoka mwishoni mwa mwaka huu.
0 maoni:
Chapisha Maoni