Huu ni ujumbe wa Beyonce juu ya mauaji ya watu weusi yaliyotokea Marekani

Beyonce ameonesha kusikitishwa na mauaji yanayoendelea juu ya watu weusi huko Marekani.
Wiki hii nchi hiyo imekumbwa na mauaji kwa polisi wa kizungu kuwaua watu wawili weusi huko Louisiana na Minnesota kabla ya jana kundi la watu kulipiza kisasi kwa kuwaua polisi wamne huko Dallas. Mastaa kibao wa nchi hiyo wameonyeshwa kusikitishwa na mauaji hayo yaliyotokea akiwemo Queen Bey kwa kuandika ujumbe uliosema, “This is a human fight. No matter your race, gender or sexual orientation. This is a fight for anyone who feels marginalized, who is struggling for freedom and human rights.”
Hata hivyo hayo siyo mauji ya kwanza juu ya watu weusi. Mwaka jana pia yalitokea mauaji yaliyomhusisha polisi wa kizungu kwa kumuua mtoto mweusi.

0 maoni:

Chapisha Maoni