Dj Khaled amsifia Kendrick Lamar kwenye wimbo wake ‘Holy Key’
Dj Khaled amesifia mashairi ya Kendrick Lamar kwenye wimbo wake mpya ‘Holy Key’.Kwenye wimbo huo Dj Khaled amewashirikisha Big Sean, Kendrick Lamar na Betty Wright na anatarajia kuuachia kwa mara ya kwanza Ijumaa hii kwenye mtandao wa Apple Music. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Dj Khaled amesema, “Kendrick Lamar went so hard. His verse I feel like is gonna be one of the most-talked-about verses.”
Wimbo huo ni miongoni mwa nyimbo zilizopo kwenye albamu mpya ya Dj Khaled ‘Major Key’ inayotarajiwa kuachiwa Julai 29 mwaka huu.
0 maoni:
Chapisha Maoni