Izzo bizness awapa shavu Jfish Julius Hunter Nyandindi na patrick alisina kutokea mbeya

msanii na mkali wa miondoko ya hip hop anayetamba na ngoma yake ya dangerouz boy aliyo mshirikisha mwanadada makini sana abela music anayetokea kwenye kundi la the amaizing linalomilikiwa na rappa huyo kutokea mbeya.
Hivi karibuni rapa huyo alijaribu kutoa mchango wake katika sanaa ya muziki kwa kuwapa sapota wakali wawili wanaofanya vizuri nyanda za juu kusini hususani pande za mbeya ambako rapa huyo ndiko alikoanzia katika harakati zake kimziki. katika mtandao wa instagram rapa huyo aliandika haya
pia kama wewe ni mdau wa kazi za sanaa unaweza kutoa mchango wako kusapoti mziki wa wasanii hawa.

0 maoni:

Chapisha Maoni

lijue kundi hili kutokea mbeya (FIVE GROUND UNIT)

kwa kutazama kutazama interview hii kutoka MICHUZI TV utaweza kuona maana halisi ya muziki wao
lipokee kundi hili kwa mashiko na upendo wa dhati kwa kulipa nguvu ili lifike mbali katika sanaa ya muziki wa tanzania. shukrani na sapoti muziki mzuri kwa namna moja ama nyingine kutoka kwa hawa jamaa

0 maoni:

Chapisha Maoni

Jfish Julius Hunter Nyandindi kutokea mbeya ameunda kundi jipya la kazi za muziki N-S-B

Jfish Julius Hunter Nyandindi ni msanii anae fanya vizuri katika sanaa ya muziki wa hip hop nyanda za juu kusini na tanzania hivi karibuni alitangaza ujio wa kundi jipya katika tasnia ya muziki wa hip hop nchini.
Msanii huyo aliyasema haya katika mitandao ya kijamii "Napenda kutambulisha rasmi kundi langu la N-S-B likiwa limejumuisha watu watano 1- J. FISH 2-MARKMOSH 3-TAIVINA 4-B. DESGNER 5-MAALIM SBK Na hiyo ndo list sahihi ya crew yangu Kama unahisi unaweza vizuri mziki hakika nitafute tutashirikiana kwa mengi BY N-S-B PRESDENT ‪#‎MGUU‬. Wa. ‪#‎SIMBA‬"
aidha msanii huyo amejaribu kuwahakikishia mashabiki wa muziki wake watarajie makubwa kutoka katika kundi hilo na anawaomba muendelee kumsapoti katika kazi zake na kundi lake hilo jipya

1 maoni:

Chapisha Maoni

Waziri Nape nauye ashiriki kuupokea mwili wa marehemu Joseph Senga Airport dar

Moja ya headline iliyotawala July 28 2016 katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ilikuwa ni pamoja na hii ya kutokea nchini India iliyohusu kifo cha mpiga picha wa Gazeri la Tanzania Daima Joseph Senga aliyefariki akiwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Marehemu Joseph Senga ndiye mpiga picha aliyenasa tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha talevisheni CHANEL 10 Daud Mwangosi kilichotokea September 2 2012 katika kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Leo July 30 2016 mwili wa marehemu Joseph Senga tayari umewasili nchini ukitokea India, ambapo Waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Nape Nnauye aliungana na baadhi ya watanzania wakiwemo wapiga picha wenzake wa kutokea vyombo mbalimbali vya habari. Na hizi ni picha zingine za mapokezi ya mwili wa marehemu.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Sallam atoa hint ya ujio wa album mpya ya Diamond

Kuna uwezekano mkubwa kuwa Diamond anajiandaa k
uachia album yake mpya. Meneja wa staa huyo ambaye kwa sasa yupo Afrika Kusini ametupa hint kuwa santuri mpya ya msanii wake ipo njiani kuja. Sallam Sharaff amepost picha hiyo chini na kuandika kwa maneno yanayotafsiriwa kwa Kiswahili ‘hii ni tarehe sahihi ya kuachia album.’
Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake Kidogo aliowashirikisha P-Square. Video ya wimbo huo hadi sasa ina zaidi ya views milioni 2.2 kwenye Youtube.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Koffi Olomide aendelea kusota, anyimwa dhamana

Mwanamuziki maarufu Koffi Olomide amenyimwa dhamana ya kuachiliwa huru kulingana na wakili wake.
Muimbaji huyo baada ya kupandishwa mahakamani alikanusha tuhuma zinazo mkabili huku jaji alikataa ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana. Siku ya Jumatatu ,maafisa wa polisi walimkamata Olomide mwenye umri wa miaka 60 nyumbani kwake katika makaazi ya Kinshasa baada ya kupatikana katika kamera akimpiga teke mmoja wa wanenguaji wake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini nairobi. Alirejeshwa nchini DRC kutoka Kenya kufuatia kisa hicho cha Ijumaa. Hatua hiyo ilisababisha kufutiliwa mbali kwa tamasha lake nchini Kenya na Zambia. Source: BBC

0 maoni:

Chapisha Maoni

Nyangumi nusura azamishe boti la watalii

Ni mandhari ya kupendeza sana... Utadhani maonyesho.. Ni wakati nyangumi mmoja aliporuka juu kutoka ndani ya maji ,mita chache tu kutoka mahali boti moja ya watalii ilipokuwa inapita. Nyangumi kumi na wawili walikuwa wakiogolea karibu na ufuo wa pwani ya kaskazini mwa Sydney nchini Australia.
Ulikuwa wakati wa msimu wa nyangumi hao kuhama kutoka sehemu moja ya bahari ya Australia hadi nyengine. John Goodridge ni mmoja waliokuwa wakitazama mwenendo wa nyangumi wakati alipopiga picha hiyo yakuvutia akiwa katika boti nyengine umbali wa mita 500. ‘Kwangu mimi , lilikuwa tukio la kufurahisha, na kuchekesha lakini najua kwaoyaaani watalii hao lilikuwa tukio la kushtusha kweli! Kwani wakati nyangumi huyo alipofanya hivyo boti lao liliyumba utadhani ni kifiniko cha chupa baharini' John Goodridge ameelezeaNyangumi huyo alikuwa na uwezo ha kulitosa boti hilo na pamoja nayo maisha ya makumi ya watalii ,mnyama huyo alikuwa ni mkubwa sana. Maelfu ya nyangumi wanaelekea Queensland ambako msimu ni baridi zaidi huko. Viumbe hao wa kuvutia wanatarajiwa kurudi tena bahari ya Antarctic kutoka Septemba hadi Novemba. "Mara nyingi nyangumi huwa wanashangaa kuona boti baharini lakini ni nadra kwamba wataziandama na kuruka ruka karibu ya vyombo vya baharini,"

0 maoni:

Chapisha Maoni

Ripoti:Man United yamnyakua Pogpa kwa uhamisho unaovunja rekodi ya dunia

Manchester United imekamilisha dili la kumsainisha mshambuliaji wa Juventus, Paul Pogba kwa uhamisho unaovunja rekodi ya dunia, paundi milioni 100.
Mtandao wa Daily Mirror umeripoti kuwa United imekubali kuwalipa Juventus kiasi hicho kikubwa cha fedha ili kumchukua staa huyo wa Ufaransa kwa mkataba wa miaka mitano atakaokuwa akilipwa £210,000 kwa wiki. Kocha wa United, Jose Mourinho, alihakikisha kuwa Pogba anajiunga na timu yake baada ya kuisaidia timu yake ya taifa Ufaransa kuingia fainali ya kombe la Euro 2016. Chini ni uhamisho mwingine uliokuwa wa gharama zaidi katika soka.

0 maoni:

Chapisha Maoni

‘The little boy is a public property’ asema Huddah, aingia kwenye beef na Zari, kisa Diamond

Kila kukicha, drama mpya inazaliwa na Diamond anakuwa centre ya ubuyu.
Staa huyo alifanikiwa kuizima skendo ya kumsaliti mpenzi wake Zari kwa kudaiwa kutembea na Hamisa Mobetto kwa kuachia hit yake ‘Kidogo’ na P-Square, lakini jingine limeibuka tena wiki hii. La sasa hivi limhusu Zari na staa wa Kenya mwenye skendo chungu mzima, Huddah Monroe na kila mtu anajiuliza limeanzia wapi!
Ni kwasababu mastaa hawa walikuwa marafiki siku za nyuma. Let’s guess tatizo limeanza baada ya kudaiwa kuwa Zari amemkaushia Huddah kumpa mwaliko kwenye birthday party ya mtoto wake, Tiffah itakayofanyika mwezi ujao. Ikumbukwe kuwa, June mwaka huu Huddah alipost Instagram kuelezea jinsi alivyo na hamu na birthday ya binti huyo maarufu. “Our baby @princess_tiffah Turning ONE soon…. The ROYAL DUTCHESS of TZEE . Hii Sio party ya kikosa Jamani . There will be a BIG SURPRISE that day! Asiye na wake aeleke jiwe….Mimi I’ll be there na mawe zangu khaa! Mama Tiffa @zarithebosslady give us LOCATION Basi …. We need to book tickets EARLY,” aliandika Huddah. Lakini katika badiliko kubwa la tukio, ni hasimu wake na Huddah, Vera Sidika ndiye anadaiwa kualikwa. “Finally, Countdown to Tiffah’s Birthday. I’m so excited kuja vile mnajua itakuwa mambo moto, Kama vile White Party,” ameandika Vera kwenye Instagram. “As u know your parents @zarithebosslady @diamondplatnumz hawakosei wakifanya kitu. Wacha nichukue hii nafasi kusema HAPPY BIRTHDAY @princess_tiffah wangu Mungu akutunze na kukupa afya njema na ukue vyema aunty Vera anakupenda sana na amekununulia zawadi najua utayafurahia,” ameongeza. “Kama na wewe utakuwa mmoja wapo kwa walioalikwa basi itakuwa bomba sana maana patakuwa apatoshiiii yani na Kama ujaalikwa ni tatizo maana kule ni shidaaaaaa😆. Watu na aunty Zao. Wacha niishie hapa Tukutane huko.” Japo kunaweza kuwa na sababu nyingine kubwa zaidi nyuma ya mtifuano huo, lakini Huddah ameonekana kumind na amemrushia Zari makombora mfululizo kwenye Snapchat. Kwa mujibu wa bidada huyo, Diamond ni mali ya umma inayoweza kugawiwa na mtu yeyote kama pizza. Kwenye ujumbe mwingine ameeleza kuwa amewahi kula chakula na wote wawili akiwaenjoy tu. “When you think your man is yours kumbe he is ours. And I ate and dined w both of u,” ameandika Huddah. “LOL. Having kids with someone to tie him down doesn’t mean he won’t leave,” ameandika kwenye snap nyingine. Tazama snapchat zote hapo chini.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Urusi yafungiwa kushiriki michezo ya Olimpiki 2016 huko Brazil

Wanariadha wa Urusi hawatashiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka huu huko Brazil. Kauli hiyo imeafikiwa na mahakama ya juu ya michezo ambayo imefutilia mbali rufaa iliyowasilishwa na kamati ya olimpiki ya Urusi ROC ya kuitaka ibatilishe uamuzi wa shirikisho la riadha duniani IAAF wa kuwapiga marufuku wanariadha wake
wote wasishiriki michezo ya olimpiki itakayoandaliwa jijini Rio De Jenairo Brazil kuanzia mwezi ujao. IAAF ilifikia uamuzi huo baada ya ufichuzi kuwa serikali ya Urusi ilikuwa na mpango wa chini kwa chini wa kuficha matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku miongoni mwa wanariadha wake. Kamati ya olimpiki ya Urusi ilikuwa imekata rufaa kwa pamoja na takriban wanariadha 68 ambao hawajawahi kupatikana na hatia ya matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini. Baada ya kusikiza pande zote mbili mahakama hiyo ya juu katika riadha CAS imeamua kufutilia mbali rufaa hiyo. Kauli hiyo imewadia siku moja tu baada ya uchunguzi huru kubaini kuwa wizara ya michezo ya Urusi, na kamati ya kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini ya Urusi zilishiriki udanganyifu ikiwemo kubadilisha mikojo ya wanariadha ilivipimo visipatikane na madawa hayo yaliyopigwa marufuku. Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC imesema itatathmini kwanza hatua za kisheria, kabla ya kufanya uamuzi wowote kuhusu iwapo itaipiga marufuku Urusi kutoka kwenye mashindano ya Olimpiki huko Rio de Janeiro Brazil. Hatua hii inafuatia ripoti huru kuhusu serikali kuhusika na kuwasaidia wanamichezo wake katika matumizi ya madawa ya kusisimua misuli. IOC hata hivyo imewafungia maafisa wote wa Urusi kushiriki michuano ya Olimpiki ya Rio, na itawapima tena wanamichezo walioshiriki michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi yaliyofanyika Sochi. Tayari wanariadha wa Urusi wamepigwa marufuku na IAAF. Shirikisho la riadha IAAF limefurahia kauli hiyo ya mahakama ya juu ya michezo ikisema kuwa imesawazisha uwanja wa riadha. ”Kwa hakika tumefurahi kuwa CAS imeunga mkono kauli yetu. Leo kwa hakika sio siku ya kufurahia kwani IAAF haikuja katika michezo kuwazuia wanariadha wasishiriki katika michezo ila nia yetu ni kusawazisha uwanja ili wanariadha wote washindane kw mizani sawa” alisema rais wa shirikisho la riadha Lord Sebastian Coe. ”Baada ya rio tutaendelea kuisaidia kamati ya olimpiki ya urusi ilikuwaruhusu wanariadha wake kurejea katika mashindano ya kimataifa.” aliongezea Coe. Licha ya uamuzi huo wa CAS,wanariadha wachache wa urusi ambao watakubali kushiriki chini ya bendera ya kamati ya olimpiki wataruhusiwa kushiriki ila lazima wapitie vipimo za ziada ilikuthibitisha kuwa ni wasafi. Source: BBC

0 maoni:

Chapisha Maoni

Rapper Kid Cudi kuonekana katika msimu mpya wa ‘Empire’

Rapper Kid Cudi amepata shavu la kuonekana kwenye show kubwa ya muziki na maisha ya “Empire.” Staa huyu ataigiza kama Gram, rapper ambaye hana lebo na atakuwa mpinzani mkubwa wa Hakeem (Bryshere “Yazz” Gray) kwenye studio na kwenye maisha.
Gram pia atakuwa ana mahusiano na Ex wa Hakeem, Tiana (Serayah McNeill) katika Empire. Kipindi cha nyuma Kid Cudi aliwahi kuigiza kwenye filamu kama Entourage na James White. Msimu huu tatu wa Empire utaanza kuonekana kuanzia Sept. 21, huku pia wakiwemo French Montana na Birdman.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Dj Khaled amsifia Kendrick Lamar kwenye wimbo wake ‘Holy Key’

Dj Khaled amesifia mashairi ya Kendrick Lamar kwenye wimbo wake mpya ‘Holy Key’.
Kwenye wimbo huo Dj Khaled amewashirikisha Big Sean, Kendrick Lamar na Betty Wright na anatarajia kuuachia kwa mara ya kwanza Ijumaa hii kwenye mtandao wa Apple Music. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Dj Khaled amesema, “Kendrick Lamar went so hard. His verse I feel like is gonna be one of the most-talked-about verses.” Wimbo huo ni miongoni mwa nyimbo zilizopo kwenye albamu mpya ya Dj Khaled ‘Major Key’ inayotarajiwa kuachiwa Julai 29 mwaka huu.

0 maoni:

Chapisha Maoni

ZAX 4REAL kutengeneza umoja wa wasanii kama kundi mbeya.

Umoja wa kundi hilo linajulikana kama "FIVE GROUND UNITY" Umoja huo umejumuisha wasanii wanne(4)ambao ni:ZAX 4REAL,HOPE MUSIC,IQ DE MUSIC na CANDY DIVAH. Kwa ufupi tegemeeeni mapinduzi ya mziki kutoka kwa "FIVE GROUND UNITY"kwa mambo mazuri tuliyojipanga kuyafanya ktk game la mziki TANZANIA ahsanteni
ZAX 4REAL mmojawapo wa wasanii wa kundi hilo
Anaitwa ‪#‎CANDYDIVAH‬ mmoja kati ya @five_ground_unity tegemea maajabu atayo yafanya ktk umoja wa kundi hili la @five_ground_unity...ni bidada mwenye sauti nzuri sana kiufupi tegemea makubwa kutoka kwake na kundi zima la @five_ground_unity..mwite ‪#‎firstlady

0 maoni:

Chapisha Maoni

VIDEO Zax B Mtoto wa Boss HQ

0 maoni:

Chapisha Maoni

Picha: Utaupenda ujumbe wa Lulu akiwa na Majay

Mshindi wa tuzo ya AMVCA 2016, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na CEO wa EFM, Dj Majay, wameamua kuuonyesha umma ni jinsi gani wako karibu zaidi.
Wawili hao ambao kwa sasa mahusiano yao yako wazi zaidi, wamekuwa wakishare picha mbalimbali wakiwa pamoja katika mitandao ya kijamii na kuonyesha jinsi wanapendana.
Hapo awali, Majay alikuwa anatoka kimapenzi na Hamisa Mobeto na walibahatika kupata mtoto wa kike, Fantasia.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Picha,Mashabiki walalamikia mavazi ya Serena Williams kifuani,washindwa kutazama mechi sababu ya…..

Baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye michuano ya Wimbledon Serena Williams ameanza kupambana tena na kauli za mashabiki kuhusu Chuchu zake za maziwa kuonekana kwenye nguo yake wakati anacheza.
Mashabiki wamelalamika twitter kuwa walishindwa kuangalia mchezo vizuri sababu ya kutazama Chuchu za ‘Serena Williams’ Hata baada ya kuweka rekodi mpya kwenye mechi hio kwa ushindi mkubwa wa muda mfupi kuliko wowote uliowahi kutokea kwneye michuano hii kwa kumshinda mrusi Elena Vesnina 6-2, 6-0 ndani ya dakika 49, ila watu bado walilalamikia kifua chake. Hizi ni picha za kifua chake na twits za watu wakilalamika.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kwa mujibu wa Life & Style, rapa Kanye West ametumia zaidi ya bilioni moja ya pesa za Tanzania kutayarisha video ya Famous.
Kanye West ametumia dola za kimarekani $750,000 kwajili ya kutengeneza sanamu za mastaa walioonekana kwenye video yake hio maarufu zaidi duniani. Repoti hii inasema sanamu za mastaa hawa zimechukua zaidi ya mwaka mmoja kukamilika huku wafanya kazi wakali wa Kanye West wakisimamia kazi yote. Mastaa wanaonekana watupu kwenye video ya Kanye ni pamoja na Caitlyn Jenner,Kim Kardashian, Ray J, Taylor Swift, Rihanna, Chris Brown, Donald Trump, Caitlyn Jenner, Bill Cosby, George W Bush na Amber Rose.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Afande Sele asema amechoka maisha ya ukapera

Baada ya hivi karibuni rapper kutokea Morogoro, Afande Sele kudai kuwa hana mpango wa kufunga ndoa, Jumatano hii ametengua kauli hiyo kwa kudai kuwa amechoka maisha ya ukapera.
Rapper huyo ambaye kwa sasa ana jukumu la kuwalewa watoto wake wawili ambao mama yao alishafariki dunia, ameonyesha kuchoshwa na kazi mbalimbali za nyumbani ambazo analazimika kuzifanya. “Najisikia kuoa tena,” alisema Afande. “Mara chache huamua kula kwenye sufuria kwa sababu naishi mwenyewe hivyo napika mwenyewe, naosha vyombo mwenyewe nk, hivyo kwasababu ya uvivu wangu katika kuosha vyombo wakati flani huamua kula kwenye sufuria ili kuepuka kuchafua vyombo zaid pasi na ulazima,” aliandika kupitia facebook yake. Hivi karibuni alikaririwa na chombo kimoja cha habari akidai kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kumtafuta mwanamke sahihi ambaye atafanya naye maisha.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Ciara asema mume wake anampe mambo flani vizuri sana.

Russell Wilson anaonekana kuwa mtu aliyefanikiwa kwenye kila alichotaka kitokee kwenye usiku wa harusi yake na Ciara.
Russell na Cici walifunga ndoa Uingereza mjini Liverpool na baadae Cici aliweka video fupi snapchat akiongelea usiku wake wa kwanza na mume wake huku akisema “Amepewa mambo mazuri sana kitandani” Video hio iliwekwa baada ya tetesi kuwa hawakuwa na raha baada ya kufunga ndoa kutokana na ugomvi uliotokea chumbani kwao.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Huu ni ujumbe wa Beyonce juu ya mauaji ya watu weusi yaliyotokea Marekani

Beyonce ameonesha kusikitishwa na mauaji yanayoendelea juu ya watu weusi huko Marekani.
Wiki hii nchi hiyo imekumbwa na mauaji kwa polisi wa kizungu kuwaua watu wawili weusi huko Louisiana na Minnesota kabla ya jana kundi la watu kulipiza kisasi kwa kuwaua polisi wamne huko Dallas. Mastaa kibao wa nchi hiyo wameonyeshwa kusikitishwa na mauaji hayo yaliyotokea akiwemo Queen Bey kwa kuandika ujumbe uliosema, “This is a human fight. No matter your race, gender or sexual orientation. This is a fight for anyone who feels marginalized, who is struggling for freedom and human rights.”
Hata hivyo hayo siyo mauji ya kwanza juu ya watu weusi. Mwaka jana pia yalitokea mauaji yaliyomhusisha polisi wa kizungu kwa kumuua mtoto mweusi.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Picha,Zawadi kubwa aliyopewa Kobe Bryant na rapa Snoop Dogg.

Rapa Snoop Dogg ni miongoni mwa mashabiki wakubwa wa mpira wa kikapu NBA nchini Marekani haswa timu ya Lakers na mchezaji wake kipenzi alikuwa Kobe Bryant. Baada ya Kobe aka Black Mamba kutangaza kustaa kwa kusema ‘Mamba Out’ Snoop amempa gari classic staa huyu ambalo lina picha ya Snoop akiwa amevalia jezi ya Lakers na kushikilia kikapu cha Larry O’Brien. Gari hili lina rangi za Laker nje na ndani na wakati anapewa Snoop aliandika Instagram “The gift that keeps on giving,Enjoy it mamba.”

0 maoni:

Chapisha Maoni