Sauti Sol hawatomuimba Rais Magufuli sema kuna kitu wamemkubali
Sauti Sol ni kundi la waimbaji wakali wa
muziki wa kizazi kipya kutokea Kenya, ngoma zao zilianza kuwashika
Watanzania toka kitambo mpaka sasa na moja ya ngoma zao zilizolia sana
Tanzania ni ‘sura yako’
Pamoja na kwamba wanadili sana na muziki
haimaanishi kwamba hawafatilii siasa, wameanza kuzifatilia siasa za
Tanzania kwa ukaribu zaidi baada ya kusikia kuhusu Rais Magufuli.
wamesema…‘Tunapenda
utendaji wake, Tanzania mkiendelea hivyo mtafika mbali sana, mimi
aliniacha hoi pale alipofika Airport kukagua tu mara hii mashine
imekuaje yaani huyu mzee yuko serious kuhakikisha rushwa haipo’
‘Kwa
Afrika kupambana na vitu kama rushwa lazima tuwe na kiongozi kama huyu,
na hata kabla ya Magufuli hajawa Rais alikua waziri wa ujenzi na
tulikua tunamuheshimu sana na tulikua tunasikia kwamba Tanzania kuna
Waziri flani, yani sifa zake zimeenea‘ – Sauti Sol
0 maoni:
Chapisha Maoni