R.Kelly alikaribia kumsainisha Kanye West kipindi hajatoka

Kama mambo yangeenda kama yalivyokuwa yamepangwa, Kanye West angekuwa msanii wa R.Kelly.
Kwenye interview ya hivi karibuni na BBC Radio, Yeezy alidai kuwa hicho kilikuwa kipindi kigumu zaidi kwenye maisha yake.
“Nilikuwa high school na nilikuwa nimefukuzwa kazini, au pindi nilipomchezea R. Kelly nyimbo zangu, aliniambia angenisainisha na kisha miezi mitatu baadaye, sikuwa na hela yoyote, sikuweza kumudu fedha ya kunyolea nywele, sikuweza kumpeleka demu wangu kwenye sinema, na nipo kwenye kitanda cha mama yangu, nikitengeneza beats na nilikuwa kidogo tu nisanishwe na R. Kelly,”alisema.
Hata hivyo Kanye alikuja kuwa mmoja wa watayarishaji muhimu wa Jay Z kabla ya kuja kuwa rapper mwenye mafanikio na ushawishi mkubwa duniani.

0 maoni:

Chapisha Maoni