JUSTIN BIEBER ampotezea DONALD TRUMP

Mwanamuziki nyota wa Marekani Justin Bieber amekataa kufanya show iliyoandaliwa na Chama cha Republican katika mkutano wake uliofanyika hivi majuzi huko Cleveland U.S.A.

Bieber aliitosa ofa ya dola milioni tano ambacho ni kiasi kikubwa mno kulipwa msanii kwa show moja. Lakini inasemekana chanzo cha kuitosa ofa hiyo ya Trump ni meneja wake Bieber Scooter Braun ambaye anatajwa kuwa shabiki mkubwa wa Mgombea wa Urais wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton.


Scooter alitishia kujiondoa kuwa meneja wa Bieber endapo angekubali kwenda kutumbuiza kwenye mkutano huo, hata hivyo si meneja wake Bieber tu aliyemshauri kuitosa ofa hiyo, yupo mcheza kikapu maarufu LeBron James naye alimshauri Bieber kuitosa ofa hiyo.

Inasemekana kuwa show hiyo haikuwa ya kisiasa lakini hilo halikutosha kumshawishi Bieber kukubaliana na ombi hilo.

0 maoni:

Chapisha Maoni