Bado nina mipango na Fabregas - Antonio Conte
Kocha wa Chelsea Antonio Conte, amesema kiungo Cesc Fabregas bado ana
mipango naye licha ya kutompanga kwenye mchezo wa jana wa ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya West Ham, katika uwanja wa Stamford Bridge.
![]() |
Cesc Fabregas |
Bao
la Costa, kunako dakika ya 89, liliihakikishia Chelsea pointi 3 muhimu,
baada ya James Collins, kusawazishia West Ham, wakati Eden Hazard
alikuwa ameshaandika bao la kwanza kwa The Blues kwa njia ya peanati.
"Inaweza kutokea kwa mchezaji yoyote kumwacha kwenye kikosi cha kwanza, kama nilivyomwacha Fabregas, muhimu kuona hilo ni jambo jema, kwa sababu ni lazima tupigane kwenye msimu huu, na muhimu kukaa pamoja kwa kila hali".Alisema Conte.
Fabregas aliyeachwa kwenye benchi, amekuwa akihusishwa na kutaka kutimka kwenye klabu hiyo ya darajani ambapo inasemakana huenda akakimbilia vilabu vya Real Madrid, Juventus au klabu yake ya zamani, Barcelona

0 maoni:
Chapisha Maoni