RAIS DKT. MAGUFULI AWAJULIA HALI SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI PAMOJA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN SAMUEL MALECELA JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa
furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada
ya kuwasili nyumbani kwake Sala sala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo
na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake
Sala sala jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia hali.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake
Mama Janeth Magufuli kushoto akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam
walipokwenda kumjulia hali. Kulia ni mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada
ya kuwasili nyumbani kwa Spika Sala sala jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali
Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es
Salaam.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu mstaafu John Samuel
Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akiongoza Sala ya kumuombea Waziri Mkuu mstaafu John Samwel Malecela pamoja na
mkewe Anne Kilango Malecela.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai
wakati alipokwenda na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwajulia hali nyumbani
kwao Sala sala jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mke wa
Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana
na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya
kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
0 maoni:
Chapisha Maoni