je ni kweli Mwimbaji Emmanuel Mbasha karudiana na Flora Mbasha majibu haya hapa.......
Kama utakuwa unakumbuka mnamo September 21,2015 moja ya
stori kubwa iliyogusa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania ni ishu ya
Hukumu ya Kesi ya Mwimbaji wa Gospel Tanzania, Emmanuel Mbasha ambapo
alikuwa anakabiliwa na Keshi ya kumbaka shemeji yake na kesi imekuwa
Mahakamani tangu 2014.
wengi tunafahamu kwamba mwimbaji huyo
aliachiwa huru baada ya Mahakama kumkuta hana hatia kwenye Kesi hiyo,
sasa leo kajibu swali kuhusu kurudiana na mkewe Flora Mbasha na
kuyaongea haya>>
‘Mimi kurudiana na Flora Mbasha
ni ngumu kwasababu yeye ndio aliniacha mimi na yeye ndio aliandaa
mazingira yake ya kuniacha mimi mpaka ikafika wakati Familia yangu,
viongozi mbalimbali wa Dini wakawa wanamshauri lakini akutaka kurudiana
na mimi kwahiyo naweza sema ni ngumu kurudiana na Flora’
0 maoni:
Chapisha Maoni