Rais Magufuli atema cheche Geita

Rais Dkt John Magufuli amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya mkoa hadi vitongoji kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya elimu bila malipo kwa lengo la kuthibiti mianya na matumizi mabaya ya fedha hizo.
Ameyasema hayo mkoani Geita katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mnadani mkoani Geita. Hata hivyo baada ya wabunge hao kuzungumzia changamoto zilizopo kwao Rais Magufuli aliongea na wananchi na viongozi mambo kadha wa kadha.
“Wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa , wakurugenzi waanze sasa kuweka macho yao kwa wakuu wa shule pale wanapopeleka fedha hizo ninachofahamu wapo baadhi ya walimu wanaoandika wanafunzi hewa ili kusudi wapewe pesa nyingi. Napenda nitoe wito kwa walimu wote Tanzania nzima mnatafuta matatizo, narudia tena mnatafuta matatizo msijaribu kula hela ya serikali,” alisema.
Pia aliwataka madiwani kuangalia sheria kandamizi za wafanyabiashara.
“Mkaangalie zile sheria kandamizi kwa wafanyabiashara, nina taka watu walipe kodi kwenye maduka, mtu amepita na fuso amejaza alipe kodi, mtu amebeba kambuzi kadogo kwenda kwenye mnada napo alipe? Mtu amebeba kagunia kadogo naye pia alipe? Msikubali kupelekeshwa tujenge mazingira rafiki kwa watanzania wanyonge.”
Kwa upande wake Naibu waziri wa nishati na madini Dk Mellard Kalimani, alimhakikishia Rais kuwa umeme utapatikana wa uhakika huku akisema, “hasa kwa kiwango chako mheshimiwa Rais umeme haupo kwa kiwango chako. Lakini mheshimiwa rais nikuhakikishie kwa mipango yako na ilani ya chama cha mapinduzi umeme katika mkoa wote utafika hadi kwenye vitongoji.”
Naye mbunge wa Busanda Lolensia Bukimba, alipata fursa ya kusalimia mkutano huo na kutoa maombi, “Tuna tatizo la maji, tuna changamoto kubwa ya maji tunataka maji yatoke ziwa Victoria yatufikie wananchi na kama unavyoona mji wetu unakuwa kila siku hivyo maji ni muhimu kupatikana na pia tunahitaji rasmi ili watu waweze kufanya biashara zao.”
CHANZO:TBC
BY: EMMY MWAIPOPO

0 maoni:

Chapisha Maoni