Hatimaye maombi na dua za mashabiki wa kundi la P-Square yamekamilika
baada ya ujumbe wa Paul Okoye kuonyesha kurudi upya kwa kundi hilo.
Ni muda mrefu umepita tangu kundi hilo linaloundwa na ndugu wawili
ambao ni Peter na Paul Okoye kuvunjika na kila mmoja kufanya kazi
kivyake. Wakati wa kuvunjika kundi hilo Peter aliachia wimbo wake wa
kwanza akiwa mwenyewe ‘Kiss Kiss’ na ‘Look Into My Eyes’ huku akitumia
jina la Mr P na Paul alianza kutumia jina la Rude Boy huku akifungua
lebo yake iliyokuwa ikiwasimamia wasanii wawili.
Hakika baada ya hatua hiyo muziki wa Nigeria ulionekana kukosa ladha
kama tomato unapoikosa kwenye kiepe japo haishibishi hata ukiikosa
lakini utatamani kukirudisha kwa muuzaji.
Paul alionekana mara kadhaa kuchukizwa kuvunjika kwa kundi hilo huku
akimuomba ndugu yake warudi wafanye kazi kwa pamoja kama zamani lakini
kwa wakati huo ilishindikana. “Mpendwa kaka yangu nakuomba, hata kama
humtaki tena Jude na hauitaki P-Square, milele utakuwa kaka yangu.
Lakini natamani sisi watatu tungeendelea kuwa pamoja sababu ni kitu cha
furaha,” aliwahi kuandika Paul Okoye kwenye mtandao wake wa Instagram.
“Watu wanatupenda sana si sababu tu ya muziki wetu mzuri, lakini
kuwaona ndugu wakiwa pamoja, kuwa mfano mzuri kwa familia zingine na kwa
watoto wetu. Tafadhali, jishushe, samehe na sahau, bado tunaweza
kubadilisha hili jambo. Kama nilisema chochote au kufanya chochote
nilichokuumiza, nisamehe. Na kwa mashabiki wetu wote wa ukweli,
tafadhali tuombeeni. Mungu awabariki wote.”
Hata hivyo mara kadhaa Peter ameonekana kukaa kimya bila kuzungumza
chochote huku akiendelea kufanya show peke yake kwa kuzunguka nchi
kadhaa ikiwemo Dubai na nchi zingine.
Wimbo wa ‘Kidogo’ wa Diamond ndiyo ulikuwa wimbo wa kwanza wasanii
hao ndugu kuonekana mara ya kwanza kwenye video wakiwa pamoja tangu
lilipovunjika kundi lao na kuwafanya mashabiki waliowazoea kufurahia
kitendo hicho huku wakiwa na matumaini mapya ya kurudi tena kwa kundi
hilo.
Mwezi Julai mwaka huu hatimaye aliyekuwa mgumu wa kubadili maamuzi
yake, Peter alipost kipande cha video akiahidi kurudi tena na kuwaomba
radhi mashabiki wao kwa yaliyotokea lakini pia alitangaza kumrejesha
kaka yao, Jude Okoye kama meneja wao. “Something new Cooking in da
kitchen and about to come out! From us! You already know it’s P2 baby!!!
#KoolestDudes,” aliandika Peter kwenye post yake aliyoiweka kwenye
instagram hivi karibuni.
Picha mpya ya Peter na Paul Okoye waliyopiga hivi karibuni
Hatimaye Paul Okoye ameonekana kufurahia uamuzi huo wa ndugu yake na
ameonekana kumsamehe ndugu yake kwa moyo mmoja baada ya hivi karibuni
kuweka picha mbili kwenye mtandao wake wa Instagram alizopiga na ndugu
yake huyo na kuandika, “History

it’s all Good

.” “Family is everything


,” aliandika kwenye picha nyingine.
Penye nia pana njia, hakika maombi ya mashabiki hao yanaonekana
yameanza kukamilika ni muda wa kusubiri chakula wanachotuandalia huko
jikoni.
0 maoni:
Chapisha Maoni