Young Dee aanza kuona neema tangu alipoacha kutumia unga
Rapper Young Dee amesema tangu ameacha kutumia madawa ya kulevya anaona mwanga kwenye maisha yakeRapper huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, “Nilikuwa napigana vita kati ya nafsi na roho.”
“Nimeweza kushinda vita hiyo sasa hivi siitaji mwili wangu uniendeshe mimi bali mimi nasikiliza moyo wangu zaidi, na kiukweli toka nimeacha haya mambo sa hizi naona mwanga katika maisha yangu,” aliongeza.
Aidha Young Dee aliendelea kwa kusema, “Mama yangu mzazi ananipenda sana, alikuwa anasikia mambo kutoka kwa watu na mimi nilikuwa nikifika naweza labda kumuachia pesa lakini nikagundua vyote navyofanya havina thamani kwake.”











0 maoni:
Chapisha Maoni